Sunday, June 24, 2012
Kwa kuwa ndani ya kwaya ya Mt.Jeromekuna wanataaluma tofauti,Mwalimu huyu hakusita kuingia chimbo na kuwatolea nondo z maana kuhusu elimu ya mahusiano na uzazi.Ni mwalimu wa kwaya lakini kumbe amesheheni nondo za maana.Hapa akiteremsha mambo ya Rizaz fakta. kwa wale waliotoroka baiolojia jaa walionekana kidogo wakisinzia huku wengine wakianza kukosa mudi.Big up ticha.
| Hapa wanakwaya wa kwaya ya Mt.Jerome wakisikiliza kwa makini jambo kutoka kwa Mwenyekiti wao. |
Hapa Mwenyekiti wa kwaya ya Mt.Jerome akinena jambo wakati wa hafla hiyo fupi.
Kulifuatiwa pia zoezi la ugawaji wa vyeti ambapo Mgeni rasmi katika hafla hiyo fupi ,Rais wa serikali ya wanafunzi Tumaini Mr.Mauna Chuma aligawa vyeti kwa waagwa ambao ni wanakwaya wa mwaka wa tatu.
Zoezi likiendelea
Hapa dada Akwinata alikuja na staili yake kama anavyoonekana tofauti na wengine kidogo
Dah nitakumiss sana bro!!
" Kaka kweli unaondoka?!"
" Haya kila la kheri bwana!!"
Ili itifaki izingatiwe mdada huyu ilibidi apewe vyeti viwili kwa sababu wapo wawili.
"Dah saaafi sana"
" Hili litakua pozi zuri"
" Subiri tupige kwanza picha ndio uondoke dada"
Hapa zoezi limekamilika MC.TEMBA anavuta punzi kuendelea na ratiba
Njoo nikunongoneze kidogo.
Zoezi likaendelea kama ilivyoratibiwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakatoliki tumaini hakukaa kimya.
Waziri mkuu naye alikuwemo mjengoni na yeye hakusita kuonyesha hisia zake kwa kijana Maluli.
Saturday, June 23, 2012
Mimi ni John Alex.Nachukua shahada yangu ya kwanza ya uandishi wa habari lakini pia naitumia taaluma yangu.Naipenda sana kazi yangu.Kila kukicha napata mawazo mapya ya namna gani nitaifanya kazi yangu hii kwa ufanisi mkubwa.
Naamini hakuna kazi nzuri kuliko nyingine wala kazi isiyo na pesa isipokuwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii ndiko kutakuletea mafanikio unayoyawazia mbeleni. Nidhamu na uchapa kazi ndio silaha yangu.
Naamini hakuna kazi nzuri kuliko nyingine wala kazi isiyo na pesa isipokuwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii ndiko kutakuletea mafanikio unayoyawazia mbeleni. Nidhamu na uchapa kazi ndio silaha yangu.
Friday, June 15, 2012
Hatujadhamiria kupambana na umasikini nchini.
Na: John Alex.
“Kama kila mmoja wetu angefagia
nje kwake basi bila shaka dunia nzima ingekuwa safi”Haya
ni maneno ya mtawa mmoja wa dini ya kikristo kutoka dhehebu la katoliki ajulikanae
kwa jina la mama Theresa aliyewahi kuishi huko barani Asia nchini India,maneno
ambayo leo nimeona nianze nayo.
Napenda sana kutumia mifano
nikirejea maisha ya watu wa kipato cha chini ambao ndio walio wengi hapa nchini
Tanzania hususan wakulima waishio maeneo ya vijijini na kama nikiwagusa mijini
basi napendelea wale waishio uswahilini maeneo ambayo ndio yanatoa taswira ya
maisha halisi ya mtanzania.Achana na wale waishio mitaa ya Masaki,Ostabei huko Dar es salaam,na kama ni
mkoani Iringa basi waishio Wilolesi,na Igangilonga hawanihusu leo hii.
Bahatika siku moja kutembelea
maeneo ya uswahilini,halafu kule chunguza kwa makini sana maeneo ambayo watu wanapenda kukusanyika
wakiongea mambo mbali mbali,utapata majibu ambayo kwa sehemu fulani yataendana na haya ya kwangu.
Uswahilini bwana,saluni za
kiume hufurika vijana ambao asilimia
kubwa unawakuta wakisikiliza muziki wa kizazi kipya wala hawaendi kunyoa kwa
sababu wengi wao utawaona na rasta kichwani.Hii iko sana mijini tena utawakuta wengine maeneo ambayo
wameyapa majina kama vile kijiweni,kempu
saiti na kadhalika na huko unawakuta wakiburudika na bangi ambayo imepewa
majina kama vile Kaya,Widi,Mjani. na Ganja.
Kijjini nako kuna wanaume wenye nguvu zao wasio na
aibu ambao hawafanyi chochote na badala yake kuanzia asubuhi mwanzo mwisho
utawakuta wakipiga mambo yetu yale,sasa kama ni hapa Iringa au Mbeya ni Ulanzi ndio namaanisha.Kama wangekuwa Ujerumani kipindi cha Adolf
Hitler wasomaji mashahidi watu kama hawa ambao waliitwa kwa lugha ya kiingereza(unproductive)
walikuswanywa vizuri tu na kutupwa baharini ama
walichomwa moto kwenye cchumba cha gesi.Na hii iliwatia adabu wajerumani
wakati huo na matokeo yake nchi iliendelea na matokeo yake ikapata kiburi cha
kuitawala dunia fuatilia historia ya
ujerumani.
Sasa huyu mwanamke naye kaolewa na ni mama wa nyumbani,hana
shughuli yeyote ya kumuingizia kipato
kamuandaa mumewe kwenda kazini asubuhi ,kamvalisha
mtoto tayari kumpeleka kwenye
kajinasari jirani tu na nyumbani
akisharudi mwanamke hatulizi miguu nyumbani asubuhi hiyo hiyo anasugua kisigino
huyo! mpaka nyumba ya jirani,akifika kwa shoga yake wanatoa jamvi nje wanaanza
kupeana michapo na mbaya zaidi wengine
wanavuka mpaka mambo ya ndani wanashea pamoja.Aaah! ndio mambo ya wanawake
hayo. “Tutafanyaje na wakati huku mjini uswahilini nyumba zimebanana hata
kufuga kuku tu ni inshu chumba chenyewe ni kimoja”Jamani hata kuuza maandazi pia au kufuma vitambaa! kwani
kuuza genge vipi?
Kwa mtazamo wangu nafikiri elimu
ya uzazi wa mpango hususan baadhi ya maeneo huko vijijini bado kabisa haijawafikia na kama
imewafikia basi hawajaielewa sawa sawa kwa sababu inakuaje wanandoa wanazaa kila mwaka mtoto jamani?
Inafikia kipindi familia unakuta ina watoto nane na kuendelea.Kibaya zaidi
hembu kwa nje tu angalia afya ya mama na mtoto ilivyo ya kusikitisha! Mzee naye
kachoka kweli kweli anategemea biashara ya mkaa na kuwalisha watoto na mama yao
tu ni inshu siku nyingine wanashindia uji,nyumba ni ya nyasi tena wala dirisha
haina na inakaribia kuanguka mchwa washafanya kazi yao.Kali zaidi watoto watatu
wa mwisho wana shinda na chupi tu wengine ndio kidogo wana kaptura
na wa kiume wakubwa kidogo mashati ya
baba yao ya zamani ndio wanajisitiri. Choo nacho kilishajaa siku nyingi na
ukienda kusabahi hapo muda wowote angalia sana
usije ukakanyaga kinyesi cha watoto.Kwa hili nasema watanzania wote na serikali yetu hatupo siriasi na hili swala
Huyu naye anajiita sharobaro.Ni kijana, yuko stendi ya
daladala na wala sio kuwa anasubiria Gari kaja kung’aa macho tu na kushangaa
shangaa hana lolote.Anasogea kando ya barabara pembeni kidogo kuna fundi viatu.Anaanza kucheka haalafu
anasema; “Mimi bwana hata kama nimefika
darasa la saba kuna kazi nyingine kufanya ni kama kujichoresha tu mchizi
anashona viatu dah!kweli jamaa kauzu”
Hembu ona sasa hata darasa la
saba naye katika ulimwengu huu wa leo anachagua kazi eti! Kama
sio kunyonyana katika jamii ni nini huku.Kuna kauli ya wahenga inasema mtembea bure si sawa na mkaa bure. Sasa watu kama hawa ambao wanaendekeza uvivu ikiwa hawana ujuzi
wowote na wala hawataki kuwa
wabunifu,wala hawako tayari kujituma kufanya kazi kwa lengo la kuepuka
kuwa tegemezi sikosei kuuita mzigo katika jamii na serikali kwa ujumla.
Siku zote ukitaka kutoa kibanzi kilichoko ndani ya jicho la mwenzako basi ni
vema na ni jambo la busara kama ukianza
kutoa boriti jichoni mwako kwanza na
kisha uanze sasa kukitoa cha huyo mwenzio.Namaanisha nini ?Ni kwamba
wananchi wa Tanzania walio wengi tumekuwa tukiitupia lawama serikali pasipo
kukumbuka kuwa maendeleo katika taifa
hili huletwa na wananchi wenyewe na serikali ni kama msimamizi tu.
Hapa msomaji naomba unielewe
simaanishi kuwa serikali hawana mapungufu. Wanayo. tena makubwa tu.Usimamizi
mbovu wa rasili mali nchini,ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi waliokosa
uzalendo kwa taifa lao ambao wapo katika kutetea maslahi yao binafsi pasipo
kujali dhamana waliyopewa kuwatumikia
watu kwa kuzingatia haki na usawa,pamoja na rushwa kubwa iliyokithiri haya yote ni mzigo wa serikali.Sasa
mimi leo nataka kila mmoja abebe mzigo wake hapa.
Vitabu vya dini karibia zote
ulimwenguni vimekuwa vikihimiza watu
kufanya kazi kwa bidii na vingine vikiandika siri ya mafanikio ni kujituma na kinyume na hapo huwezi kufanikiwa.Sasa
kauli hii nayo inatoka katika Biblia,moja ya vitabu vya dini na inasema
“Asiyefanya kazi na asile”
Leo nataka tuangalie umasikini
kama tatizo la kijamii na nafasi ya jamii katika kupiga vita umasikini ambao
madhara yake yamekuwa yakishambulia sana
jamii za kitanzania ambazo kwa nafasi yake pia jamii hizi
zimekuwa zikijisahau kwa sehemu katika kulikabili tatizo aidha kutokana na
kutojali ama kwa kukosa tu maarifa.Aidha mchango anaoutoa mtu moja moja katika shughuli za
kujiletea maendeleo unatolewa kikamilifu?
Umasikini kama tatizo la kijamii
hugusa kila nyanja katika maisha ya binadamu ya kila siku.Hujumuisha kipato kidogo kwa wanajamii,ukosefu wa huduma
stahiki za kijamii kama vile maji umeme,hospitali,ukosefu wa mahitaji muhimu ya
binadamu kama vile chakula mavazi na
malazi lakini pia uwezo mdogo wa
kufanya maamuzi utokanao na ujinga uliokithiri miongoni mwa jamii zetu za
kitanzania,pia umasikini wa kiroho ambao humfanya mtanzania afikiri mawazo
duni,awe ni mtu wa kukata tama,,na mwenye kujiona hawezi kufanya kitu chochote.
Asilimia kubwa mtakubaliana na
mimi kuwa watanzania walio wengi katika jamii zetu tunamoishi tumeshakata tamaa na tumeridhika kabisa na
tulichonacho hata kama ni duni.Mbaya zaidi mwingine karidhika kabisa na kukosa na hatimae kujikuta tukiishi maisha
yasiyokuwa na muelekeo wowote kwani ni mara ngapi unakutana na watu waliokata
tamaa na maisha na wengi wetu tunafikiri
hawa labda wamechanganyikiwa kutokana na
muonekano wao wa nje.Hii inatokana na uwezo duni wa kufanya maamuzi.
Kwa upande wavijana katika jamiii
tunashindwa kuthubutu kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine
tunaamini kabisa kuwa hatuwezi kutokana
na mitazamo hasi ambayo imepandikizwa na waliotutangulia kwa maslahi yao.
Uvivu ni jambo ambalo linatawala
vjana wengi wa kitanzania katika dunia hii ya leo na kushindwa kufanya chochote
na ndio maana matokeo yake
tunashindwa kutumia fursa zinazojitokeza kwa manuufaa yetu wenyewe.
Zipo fursa nyingi mitaani ambazo
kwa vijana ambao kutokana na sababu
mbalimbali za msingi na zisizo za msingi wamekosa fursa ya kuendelea na masomo
yaani wameishia darasa la saba,ama kidato cha nne wanaweza kuzitumia ipasavyo
badala ya kuzidharau kujletea maendeleo ili kuepukana na tatizo kubwa la kuwa
tegemezi.
Kwa akina mama ni muda muafaka
sasa kuachana na mawazo na fikra mgando ambazo kwa maoni yangu zimepitwa na
wakati.Fikra kama vile mwanaume peke yake ndiye mtafutaji mwanamke anabaki
nyumbani.Na kwa wale dada zangu huu sio wakati wa kusubiria kuolewa kwani saasa
hivi wanaooa wanatafuta mtu anayejituma na mchapa kazi,kinyume na hapo
hutoolewa labdaumpate mvivumwenzio.Wakina dada tuepukane na hili tusije tukaishia kufanya biashara za ajabu mtaani
.Baadhi ya akina dada hawakawii.
Ni vema watanzania wakaeleweshwa
kwa mapana juu ya hali halsi ya kiuchumi namabadilikoyanayotokea ulimwenguni
kote.Katika kipindi hiki cha mabadiliko watanzania kila mmoja kwa nafasi yake
atambue nafasiyake katika kuleta maendeleo,badala ya kutegemea serikali ambaayo
na yenyewe kwa kweli inakosa muelekeo kila
kukicha
Tukumbuke kuwa sisi ni matunda ya
kizazi kilichopita na sio wafungwa wa
kizazi kilichopita.Hivyo uwezo wa kuleta mabadiliko kuanzia ngazi ya familia
kijiji mkoa na taifa upo mikononimwetu iwapo tu kila mmoja wetu
kwa nafasi yake atashiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko.
Watanzania tukumbuke kuwa nchi
nyingi ambazo leo hii ndio nchi wahisani,nchi zinazoitwa nchi zilizoendelea
zilipita katika kipindi kigumu kama hiki lakini baada ya kukubali matokeo na hatimae leo
hii wanafaidi matunda ya juhudi zao.
Nijukumu letu sasa kuhakikisha
kuwa tunaondokana na fikra za woga wa kuleta mabadiliko katika jamii,na badala
yake tuvae ujasiri tukidhamiria kuleta
maendeleo katika nyanja zote katika taifa hili.
Yote haya yatafanikiwa endapo tutarejea
na kuifanyia kazi kauli hii ya kila moja kufagia nje kwake na hatimae baadae
tutajikuta tukiishi katika Tanzania yenye siasa safi,uongozi bora na watu wote kunufaika na rasilimali za nchi
na hivyo kupata fursa sawa kwa wote kattika kushiriki ujenzi wa taifa letu
Tanzania
Miundombinu ya kisasa itapandisha hadhi vyuo vyetu Iringa.
Na;John Alex.
Mwaka jana nilibahatika kutembelea vyuo vikuu vya
Mkwawa, Ruaha na Tumaini niliko sasa, hapa mkoani Iringa kujionea hali ya vyuo
hivyo vinavyotoa elimu ya juu nchini.Sikupita kimya kimya ila nilipata fursa ya
kuongea na baadhi ya wadau wa vyuo hivyo vikuu.
Kikubwa walichokizungumza wadau
hawa ni pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili kama taasisi, lakini jambo
kubwa walilotilia mkazo ni pamoja na miundombinu haba.Uhaba wa kumbi za
kufanyia mihadhara, uhaba wa mabweni jambo ambalo kiukweli lilikuwa ni tatizo
kubwa mno.Hawakuishia hapo wadau walieleza pia mikakati na mipango mbalimbali
wanayoifanya kukabiliana na changasmoto zao huku wakitoa rai kwa taasisi hata
zisizo za kiserikali kutoa misaada
katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili kama taasisi ya kijamii.
Ilikuwa ni jambo la ajabu sana
lakini kwa hali halisi ya kitanzania hatushangai kwa sababu ndio tulivyo na
ndio uwezo wetu.Kuna baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa mkoania Iringa wamekuwa wakielekezwa kuhudhuria vipindi katika
kumbi za mikutano tena za watu binafsi ambazo hutumika kwa shughuli za harusi
na sherehe kwa ujumla.Tumefanya kumbi za sherehe madarasa ya kufanyia mihadhara
na tunalipa sawa na wanavyolipa wengine!Tutafanyaje na wakati hatujajipanga?
Wengine nao karibu asilimia 55 ya
wanafunzi wanaishi nje ya chuo na huko nako ni dhahama tupu,mara huyu
kaibiwa,mwingine kakabwa, sijasikia waliobakwa huenda wapo lakini wanaona aibu kusema.Ni eneo hili hili
wamelalamika kuwa maktaba iliyopo ni ndogo mno.Sasa mnasomea wapi? “Ahhh!
tunajibana hivyo hivyo kwenye majani kama hivi
tunalala kitabu kinakwenda si unajua mabenchi yenyewe machache”
Ni takribani mwaka mmoja
hivi umepita tangu nifanye dodoso zangu
hizo,sasa nimepita tena hivi karibuni kuchunguza je ni kweli mipango na mikakati niliyoambiwa inatekelezwa
imefikia wapi na inaendeleaje.
Kiukweli sina budi kutumia kalamu
yangu kupongeza jitihada mbalimbali
zinazofanywa na wadau hawa wa vyuo vikuu katika kukabiliana na changamoto za
uhaba wa miundombinu ya majengo.Wanajitahidi sana kwani wananchi wenyewe wanajionea kwa
macho.
Ukienda Chuo kikuu Ruaha mjini
pale utajionea namna ujenzi wa miundombinu unavyoendelea tena kwa kasi katika
maeneo ya chuoni na hii ni katika kuhakikisha wanakabilina na changamoto yao ya
uhaba wa kumbi za kufanyia mihadhara yao.Tutasoma kwenye kumbi za sherehe mpaka
lini kama si kudidimiza hadhi ya elimu na chuo kwa ujumla?
Jengo kubwa la maktaba
linaendelea kupanda kwa kasi Chuo kikuu
cha Mkwawa ili kukabilina na changamoto yetu ile ya kusomea kwenye mabenchi
tena machache kwani wengine wanalala kwenye majani ndo wanasoma.Ni
matumaini yangu kuwa hata mikakati ya ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi chuoni
hapo imefikia pazuri tu,hapana shaka.Kwa nini wasifanye jitihada na wakati wamepewa
zamana ya kusimamia na kuiendeleza taasisi?Ni kiongozi yupi asiyependa kusifiwa
kwa kuendeleza taasisi na kuifikisha
pazuri.Ah!basi tu umasikini wetu huu ndio unatuponza.
Huku Tumaini nako mambo si mabaya
kwani na wao wanajipanga kihaswa kukabiliana na tatizo hilo.Huku Tumaini kwa
mujibu wa wanafunzi wenyewe wao wanasema
hawalilii sana kukaa ndani si unajua gharama wengine zinawashinda kwa
hiyo mwaka mmoja ndani inayofwata yote nje !Ukisikia anayelilia kupata nafasi
ya kukaa ndani basi ni mgeni huyo ndo kafika.Jengo la kisasa kabisa ujenzi
unaendelea na kama inshalah panapomajaliwa likikamilika basi tutarajie kusikia
tu bwana jamaa wameanzisha kitivo kipya.Kwani ni nani asiyependa maendeleo?
Hapa nchini kwetu si jambo la
kushangaza sana kusikia taasisi Fulani ya elimu ya juu kulalamikia juu ya
miundombinu chakavu nikimaanisha majengo pamoja na vitendea kazi kama magari na
kadhalika lakini muda muafaka unapofika
sharti lazima tubuni mikakati kabambe ya kukabilinana na matatizo yetu haya ambayo kimsingi sisi ndio
chanzo.Kwani wanaozorotesha maendeleo si ni sisi wenyewe haswa pale
tunaponyweshwa pombe na kupewa fulana na kofia halafu tunawachagua kwa hiari
yetu kisha wakiharibu tunalalamika.
Sisi kama watanzania ni lazima
tuhakikishe tunachukua hatua mbadala
hususan katika kuwachagua madereva wetu ambao tunaamini watatufikisha
mahala sisi turidhike na kile wanachokifanya na hivyo tusijutie uamuzi wetu kama tunavyojuta baadhi yetu.Ni uamuzi huu pekee ndio
utazifanya hata taasisi zetu za elimu ya juu zipige hatua katika kufikia
malengo yake.
Sasa miundombinu ya kisasa katika
vyuo vyetu hapa Iringa na nchi nzima kwa ujumla ni miongoni mwa mambo mazuri
ambayo yanatarajiwa yangepewa kipaumbele sana
kiasi ambacho kama ingefanyika hivyo basi
tusingefika mahala tunalalamika oohh!
miundomibnu chakavu mara Gari la wagonjwa hakuna, hivi unafahamu kuwa yote
hutegemea uongozi mzuri?
“Mbona vyuo vingine vinatoza ada
kubwa halafu watu mmekaa kaa kimya tu kama wadudu fulani hivi!Tujiulize kwa
makini je kodi wanayotozwa kama isingekuwepo sidhani kama serikali ingevumilia
kitendo cha watu kupandisha ada kiholela.Kwa mtazamo wangu jibu ni hili; “Kama
wangetufutia kodi kabisa na tusilipe
hata kidogo basi bila shaka sisi hatupendi dhuluma,tungeshusha ada mpaka
kiwango cha chini kabisa.
Miundombinu imara ikiwemo
madarasa ya kisasa yanatoa fursa kwa wasomi wetu kusoma kwa kujiamini
zaidi,kusoma bila bugudhi yeyote na pia kuondoa kero ile ya kusoma huku watu
wakiwa wamesimama kama ilivyo katika vyuo vyetu vikuu baadhi hapa nchini kama sio hapa hapa kwetu Iringa.
Saturday, January 21, 2012
Biashara zadorora chuoni Tumaini.
Na John Alex.
Baaadhi ya wafanya biashara wa vyakula wenye migahawa na wafanya biashara zingine wanaofanya shughuli zao za biashara maeneo ya chuo kikuu Tumaini wamesema kuwa katika msimu huu wa sikukuu biashara ya vyakula na bidhaaa nyingine maeneo hayo ya chuoni imekuwa ngumu kupita kiasi.
Wakizungumza na Kwanza jamii kwa nyakati tofauti wafanya biashara hao wamesema kuwa, kufuatia likizo fupi chuoni hapo wanafunzi ambao ndio wanunuzi wakuu wa vyakula mahotelini na bidhaa nyingine wamekwenda majumbani kwao kusherehekea sikukuu ya krismasi hali inayopelekea kudorora kwa biashara na wengine kuthubutu hata kuzifunga kabisa kwa muda.
“Asilimia kubwa ya wateja wetu ni wanafunzi ambao wamekuwa wakinunua vyakula mahotelini kwa hiyo wanapoondoka inatulazimu wakati mwengine kufunga kabisa hoteli zetu kwani wanaobaki ni wachache ambao kati yao wapo wanaojipikia wenyewe” anasema Matata Elias .mmoja wa wafanya biashara mwenye mgahawa maarufu maeneo ya Tumaini ujulikanao kwa jina la Agape.
Aidha wafanyabiashra hao wamesema kuwa biashara ya vyakula na bidhaa nyingine maeneo hayo ya Tumaini huwa ni ya msimu ambapo wanafunzi wanapokuwa masomoni biashara huwa inachanganya na pindi tu wafungapo chuo wao hulazimika kufunga na hivyo shughuli za biashara kusimma kwa muda mpaka chuo kitakapofunguliwa.
Wafanya biashara hao wameongeza kuwa ugumu wa biashara chuoni hapo hususan kipindi hiki cha karibuni umechangiwa pia na kupanda kwa gharama za maisha ambapo wengi wa wanafunzi inawalazimu kubana matumizi kwa kujipikia wenyewe.
“Hata hawa wachache waliobaki hawatuungishi vizuri kwa kweli nadhani ni kwa sababu ya uchache wao na wengi kuwa wamekwenda likizo kwa hiyo wengi wetu inatulazimu kufunga biashara zetu kutokana na faida ndogo”anasema Hasani Lumato mmoja wa wafanya biashra wanaojihusisha na ukaangaji wa chipsi.
Hata hivyo kwa upande wa biahsara nyingine kama vile biashara za vifaa vya maofisini huwa ni kawaida yao pindi ifikapo muda wa likizo huwalazimu kufunga kabisa biashara zao kwani wanafunzi na wafanya kazi ambao ndio wanunuuzi wakuu wa bidhaa zao wanakuwa wamekwenda likizo na ambao wanabaki shughuli za masomo na kiofisi husimama.
Wanafunzi wa chuo cha Tumaini wamefunga likizo ndogo kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya krismas na wanatarajia kurejea masomoni mara baada ya sikukuu kuisha mwezi januari 2012.
Saturday, December 17, 2011
Mkuu wa wilaya Iringa ashauri ufugaji wa nyuki kisasa
Na John Alex.
Wananchi wa mkoa wa Iringa wameshauriwa kufuga nyuki kwa njia za kisasa na za kitaalamu zaidi ili kuweza kujikwamua kutokana na hali ngumu ya kimaisha na hivyo kupiga hatua katika vita dhidi ya umasikini na kujiletea maendeleo.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Asley Msangi katika kikao cha kamati ya ushauri (DCC)cha manispaa ya Iringa kilichofanyika mwishoni mwa wiki ilyopita katika ukumbi wa manispaa ya Iringa.
Mkuu wa wilaya amesema kuwa wapo wananchi wanaoishi kwa kutegemea ufugaji wa nyuki na hivyo ni vema wananchi wakaanzisha miradi ya ufugaji nyuki kwa njia za kisasa na za kitaalamu zaidi na hivyo kujipatia faida kupitia miradi hiyo.
Aidha mkuu wa wilaya ameishauri idara husika ya manispaa ya Iringa kuandaa mikakati madhubuti ya kuwezesha wananchi kujifunza namna ya kufuga nyuki kwa njia za kisasa na za kitaalam zaidi na hivyo kuweza kujipatia faida kubwa kutokana na mazao ya nyuki.
“Wananchi endapo wataamua kufuga nyuki kwa njia za kisasa na za kitaalamu wataweza kuinua zaidi kipato chao kwani mazao ya nyuki kama vile asali n anta yana soko sana na bei yake imekuwa ikipanda kila kukicha”alisema mkuu wa wilaya.
Amesema kuwa ni wakati muafaka kwa wananchi kuhamasika kufuga nyuki kwa njia za kisasa na za kitaalamu zaidi na kwa kushirikiana na idara husika ya nyuki ya manispaa, kuhakikisha kuwa miradi ya nyuki inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa kwani ni njia mojawapo ya kuondokana na umasikini katika taifa letu.
Mkuu wa wilaya amesema kuwa kwa muda mrefu idara husika ya nyuki ya manispaa ya Iringa imekuwa ikisuasua sana katika uhamasishaji wa miradi ya ufugaji nyuki kwani kuna muitikio mdogo sana wa wananchi katika swala zima la ufugaji wa nyuki kwa wakazi wa manispaa ya Iringa
Ameishauri idara hiyo ijifunze namna ya ufugaji nyuki kwa njia za kitaalamu na za kisasa na hivyo kuwaelimisha na kuwahamasisha wanachi ufugaji wa nyuki kwa njia za kisasa zaidi ili kuwezesha wananchi wa manispaa ya Iringa wanaojihusisha na ufugaji wa nyuki kupata kwa wingi mazao ya nyuki na hivyo kujikwamua na umasikini.
Muitikio mdogo wa wananchi:Kikwazo kwa miradi ya waitaliano Iringa.
Na John Alex.
Muitikio mdogo wa wananchi wa wa Iringa katika shughuli za miradi mbalimbali zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoendesha shughuli zake kwa ufadhili wa watu wa Italia ni changamoto kubwa inayoyakabili mashirika hayo.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki katika maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofadhiliwa na watu wa Italia waishio Mkoani Iringa yaliyofanyika katika hoteli ya Wilolesi manispaa Ya Iringa.
Katika maadhimisho hayo ambayo yalikutanisha mashirika matatu yanayofadhiliwa na waitaliano ambayo ni shirika la C.O.P.E(Coooperation for developing countries),shirika la Call Africa lenye miradi yake wilayani Iringa,na shirika la CUAM ambalo linafanya miradi yake mbalimbali ya afya mkoani Iringa.
Wadau wa miradi hiyo wamebainisha changamoto malimbali zinazowakabili katika utendaji kazi wao huku wote wakilaumu muitikio mdogo hasa wa wananchi katika shughuli za miradi mbalimbali inayofanywa na mashirika yao .
“Kumekuwa na muitikio mdogo sana wa wananchi katika shughuli zinazofanywa na miradi mbalimbali ya shirika letu la Call Africa kwa mfano akina mama wamekuwa wakikata tama katika kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kulelea watoto kama vile Kipepeo Nutritional centre ambavyo ni vya kutwa .Hali hii inawapa wakati mgumu wafadhili na ni changamoto kubwa”, anasema Lucas Marano msemaji wa Call Africa.
Kwa upande wa shirika la CUAM linalojihusisha na maswala ya afya msemaji ambae alifahamika kwa jina moja la Ricado amesema kuna changamoto kubwa sana hasa katika upatikanaji wa wataalamu wa kutosha katika kuendeleza program mbalimbali kaitka maeneo lengwa.
Aidha waitaliano hao wamebainisha changamoto nyingine zinazowakabili kuwa ni ushirikiano duni kutoka serikali kwani serikali imekuwa ikijisahau katika kutoa ushirikiano wa kutosha hususan katika kuhamasisha shughuli mbalimbali za zinazofanywa na miradi ya mashirika hayo.
Tumeandaa mabango ya usafi katika program yetu ya USAFI rafiki wa maendeleo ,wenye lengo la kuweka mji wa Iringa katika hali ya usafi lakini kwa mara kadhaa tumekuwa tukicheleweshwa na wadau manispaa tunawaomba wasiwe wazungushaji katika suala zima la utekelezaji wa miradi ya maenddeleo anasema msemaji wa Call Africa Lukas Marano.
Miradi mingine inayofanywa na mashirika hayo matatu ukiiwemo mradiwa kilimo MAWAKI na mengine mengineyo wamebainisha changamoto zinazofanana na kutaka wananchi wahamasike ili waweze kujikwamua na umasikini na kunufaika na miradi inayofanywa na mashirika haya.
Lengo la maadhimisho ni kutambulisha miradi ya waitalia wanaoishi Tanzania (wilaya za Iringa na Kilolo)kwa ajli ya watoto yatima ,walemavu,wenye mazingira magumu ,mafunzo kwa akina mama na vijana,huduma ya afya, kilimo,mifugo,ujasiriamali,na miango maalumu kuhusu UKIMWI
Thursday, December 15, 2011
MIAKA HAMSINI YA UHURU,TUTAMKUMBUKA RAIS KIKWETE KWA MIUNDOMBINU YA BARABARA.
.
Na John Alex.
Hivi karibuni watanzania tumeadhimisha miaka hamsini ya uhuru ikiwa ni tangu taifa hili lilipokombolewa kutoka katika mikono ya waingereza mnamo tarehe 9 mwezi disemba mwaka 1961 baada ya bendera ya wakoloni kushushwa pale kileleni mwa mlima Kilimanjaro na kusimikwa kwa bendera ya Taifa huru la Tanzania chini ya mwasisi baba wa taifa hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere ambaye kwa kushirikiana na wanaharakati wenzie walihakikisha kuwa taifa la Tanzania linakuwa huru na linatawaliwa na watanzania wenyewe.
Katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya TUMETHUBUTU,TUMEWEZA ,NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE wananchi wamekuwa wakitafakari kwa kina sana juu ya kauli mbiu hii kuwa ni nini tulichothubutu, ni nini tulichoweza na ni nini tunaendelea kusonga nacho mbele.Wengi wana mawazo na mitazamo tofauti .Hii inawezekana ni kutokana na itikadi zao za kisiasa ama kutofautiana tu kimtazamo kutokana na kile mtu anachoona na anachokiwaza kama sio anachokisikia.
Wasomi na wataalamu wa maswala mbalimbali walioboboea katika kufanya tafiti mbalimbali nchini wamejaribu kutoa ripoti za utafiti waliofanya na kutoa tathmini ya kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka hamsini tangu taifa hili lipate uhuru.Tathmini hizo zimegusa katika maeneo mbalimbali kama vile sekta ya afya, sekta ya elimu na maeneo mengi ambayo wataalamu hawa wamekuwa wakifanyia tathmini
.
Hata hivyo kwa mujibu wa tathmini na ripoti mbalimbali za wataalamu hawa wa maswala mbalimbali hapa nchini zimebainisha kuwa kiwango cha maendeleo kilichofikiwa hakilingani na umri wa miaka hamsini ya Taifa hili tangu lilivyokuwa huru.Kwa mfano tunapoangalia sekta ya elimu hususani swala zima la ufaulu wa wanafunzi yaani kiwango cha elimu kwa ujumla kimeshuka ukilinganisha na kipindi kilichopita.Tuachane nahayo kwani yanazidi kutukatisha tamaa
Ni dhahiri kuwa katika kipindi cha miaka yote hiyo ya uhuru hadi hivi leo,kuna mambo mengi ambayo watanzania kiukweli tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele.Kwa hayo hatuna budi kujipongeza na pia kuipongeza serikali iliyopo maarakani kwa kujitahidi kuthubutu,kuweza na mpaka sasa tunazidi kusonga mbele.
Wahenga wana msemo unaosema,Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Msemo huu una maana gani katika makala haya?Una maana kuwa,pamoja na mapungufu mengi tuliyoyaona na tuliyoyasikia kupitia vyombo vya habari kuhusu serikali, yapo mambo mazuri ambayo serikali kimsingi imeyafanya na ni sharti tuipongeze kwa uthubutu na kuonyesha kuweza.Lakini pia tunapaswa kujipongeza sisi wenyewe kwani sisi ndio walipa kodi kwa hiyo mafanikio hayo ni ya kwetu sisi hayainufaishi serikali peke yake
.
Leo nitumie fursa hii kuwaomba watanzania wote bila kujali itikadi zao za kisiasa kuwa wakweli na wawazi hasa tunapoangazia katika swala zima la miundombinu ya barabara.Kwa wale wazee wa mwaka sitini na moja ni nani wakati ule alijua kuwa angeweza kusafiri kutoka Tanga hadi Iringa kwa masasa nane tu?Ni nani wa wakati ule aliamini kuwa ipo siku Tanzania itaunganishwa na barabara za lami kwa kila mkoa?Ni nani aliamini kuwa ipo siku barabara za lami zitafika hadi vijijni?Utakapofanya utafiti utagundua kuwa wengi wahakuamini kuwa ipo siku Tanzania hii itakuwa na barabara kuu nzuri zenye kupendeza na zenye kiwango kinachotakiwa.
Leo hii kutoka Dar es salaam hadi Mbeya unahesabu masaa tofauti na kipindi kile ambapo barabara hizi zilikuwa za vumbi na zenye kutisha na yeyote anayesafiri kati ya mikoa hiyo miwili afikapo mlima Kitonga basi roho mkononi na sala zote huzisalia hapo akihofia kuwa huenda ndio mahala atakapofia kutokana na ubaya wa barabara iliyokuwepo kipindi kilichopita.
Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete imethubutu ,imeweza na inazidi kusonga mbele katika swala la miundumbinu ya barabara kwani hakuna awamu nyingine yeyote iliyopita ambayo imepata mafanikio makubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara zaidi ya awamu ya Rais Kikweteukweli ni huo.
Mikakati haiishii hapo tu bado ujenzi wa barabara za lami unaendelea kwa kasi ndani ya mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwa ni barabara za kuunganisha wilaya ndani ya mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.Haya ni mafanikio makubwa sana yaliyopatikana katika kipindi hasa cha awamu ya nne ya Rais Kikwete.Hapa turejee kauli mbiu yetu ya maadhimisho,TUNAZIDI KUSONGA MBELE.
Leo wananchi kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha miundombinu ya barabara tuthubutu kusema kuwa tutamkumbuka daima Rais Kikwete kwa kuimarisha miundombinu na si vinginevyo kwani hata kama kuna atakayefuata baada ya yeye bado yeye ndio atakuwa amefungua njia kuelekea mafanikio zaidi katika swala zima la miundombinu ya barabara.
Tukirejea hotuba ya Mh.Rais Kikwete wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru katika viwanja vya uhuru pale jijini Dar es salaam kwa ufupi tu, alisisitiza sana kuwa mafanikio yaliyopatikana katika swala zima la miundombinu ya barabara nchini ni jambo kubwa sana la kujivunia kama taifa changa linaloendelea.
Rais Kikwete alibainisha kuwa hali ilvyokuwa baada ya wakoloni kuondoka kwa upande wa miundombinu ilikuwa si ya kuridhisha hata kidogo kwani barabara za lami zilikuwa chache kama hakuna kabisa.
Hii ina maana gani? Barabara chache zilizokuwepo zilikuwa ni kwa ajili ya kusafirisha malighafi kutoka kwenye maeneo ya mashamba hadi bandarini ili kusafirisha malighafi nje ya nchi kwa hiyo hazikulenga kamwe kuwanufaisha wananchi wa Tanzania bali wao wenyewe mabepari ambao walikuwa wakitunyonya
Lakini leo barabara za lami mpaka vijijini zinajengwa mfano hai ni mkoani Kilimanjaro ambapo baadhi ya barabara za vijini zimejengwa kwa kiwango cha lami sio tu Kilimanjaro bali na maeneo mengi sana ya Tanzania, barabara za baadhi ya vijiji ni za kiwango cha lami.
Madaraja makubwa ya kuunganisha barabara hizi za kisasa yamejengwa na yaliyokuwa ya zamani yameimarishwa na kuwa ya kisasa.Mfano hai ni daraja la Mkapa lililojengwa katika kipindi cha mwishoni mwa wamu ya tatu ya Rais Mkapa, ambaloni daraja kubwa la mto rufiji.Achilia hilo kuna daraja la mto Ruvu ambalo limebadilishwa na kuimarishwa.
Ni wakati muafaka sasa baada ya kuadhimisha miaka hamsini na kutafakari kwa kina juu ya mafanikio namapungufu yaliyopatikana katika miaka hamsini ya uhuru kuachana na kutafakari mapungufu ,na kujikita zaidi katika kujua ni kwa namna gani sisi kama watanzania tunafanya nini ili kutokomeza yale mabaya nakuendeleza zaidi mazuri yaliyofikiwa japo si kitu kwa baadhi ya watu wachache wenye maslahi binafsi na chuki dhidi ya taifa letu na serikaliiliyoko madarakani ka ujumla.
Aidha ni jukumu la serikali kusahihisha mapungufu yaliyokuwepo na kuhakikisha kuwa inajipanga katika kuimarisha na kuboresha zaidi yale mafanikio mazuri ya kuridhisha yliyofikiwa katika kipindi chote walichopo madarakani na pia kuendeleza juhudi za kuimarisha mambo yote yanayoihusu kama serikali.
Pia ni jukumu la serikali kuhamasisha wananchi hususani maeneo ya kijijni kushiriki kiamilifu katika shughuli za kimaendeleo ambazo kimsingi ndizo zitalifanya taifa letu liendelee na kufikia katika kilele cha mafanikio.
Tuungane kwa pamoja katika kupiga vita maadui wanaoliyumbisha taifa hilli ambao ni ujinga maradhi na umasikini uliokithiri miongoni mwa watanzania ambao kimsingi ndio vita kuu katika taifa letu.Miaka hamsini ya uhuru tuungane kwa pamija watanzania huku tukirejea kauli ya tumesubutu,tumeweza,na tunazidi kusonga mbele katika vita dhidi ya umasikini.MIAKA HAMSINI YA UHURU,TUMETHUBUTU TUMEWEZA,NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE.
Wednesday, December 7, 2011
Mvua yahatarisha miundombinu manispaa ya Iringa.
Mojawapo ya nyumba iliyoathirika na maji Tumaini.
Na John Alex.
Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo tofauti mkoani Iringa zimepelekea baadhi ya njia kadhaa za maeneo tofauti ya manispaa ya Iringa kupitika kwa shida kutokana na kufurika kwa mifereji na vijito vya maji hali inayosababisha miundombinu ya barabara na madaraja kupoteza ubora wake na kuanza kuharibika.
Hali hii imjitokeza katika maeneo kadhaa yamanispaa ya Iringa ambapo baadhi ya maeneo hususan maeneo ya Semtema , Kihesa ,na maeneo ya chuo kikuu cha Tumaini njia zake kufurika maji wakati wa mvua hali inayopelekea wakazi wa maeneo hayo kupita kwa shida kwenye madaraja ambayo wakati wa mvua yalifurika maji.
Mvua zilizonyesha siku ya jumaatano zilifurisha mifereji na mito katika maeneo hayo hali iliyosababisha usumbufu mkubwa sana kwa wakazi wa maeneo hayo kupita kwa shida kwenye madaraja ambayo yalijaa maji na kufanya miundombinu
Aidha mvua hizo zimehatarisha baadhi ya nyumba zilizojengwa pembezoni mwa mito na mifereji kwani maji yalikaribia karibu na kuta za nyumba zilizoko kwenye maeneo ya pembezoni mwa mifereji hiyo.
Wakazi wa Semtema wamesema kuwa mvua hizo zilizonza kunyesh a hivi kariibuni endapo zitaendelea kunyesha zitaharibu miundombinu ya barabara na madaraja kwani hayakujengwa kwa kiwango kinachotakiwa kuhimili mafuriko na mvua zilizokithiri.
Hata hivyo hali hiyo imejitokeza pia katika maeneo ya Zahanati maeneo ya Mwangingo ambapo baadhi ya nyumba ziliingia maji na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa wakazi wenye nyumba zao maeneo pembezoni mwa mto kuhofia kukosa makazi baada ya kushuhudia maji yakiingia hadi ndani
.
Wakazi wa maeneo hayo wamesema kuwa endapo mvua hizo zitaendelea kunyesha zitaleta maafa makubwa ikiwa ni pamoja na kupoteza maakazi kwa wananchi waliojenga nyumba zao pembezoni mwa mito.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa manispaa ya Iringa wameliambia kwanza jamii kuwa mvua zinazoendelea kunnyesha zitapnguza ukame na hivyo kufanya shughui za kilimo kuendelea vizuri lakini endapo zitaitiliza zinaweza ziksababisha hasara kwa mazao.
Mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa bostani za mbogamboga hususan kwa wakazi wa Tumaini ambao wamekuwa wakijihusisha na kilimo cha bostani za mbogamboga pembezoni mwa mto .
Sunday, December 4, 2011
Wakaazi wa Iringa wamlilia Mr.Ebbo.
Na John Alex.
Wakazi wa mkoa wa Iringa na vitongoji vyake,wameeleza hisia zao kwa masikitiko kufuatiwa kifo cha msanii wa nyimbo za bongo fleva,mtayarishaji na mmiliki wa studio ya Motika record iliyoko mkoaniTanga Abel Motika almaarufu kama Mr.Ebbo.
Wakizungumza na Mwanahabari Halisi kwa nyakati na amzingira tofauti wananchi hao hususan vijana wameelezea kushtushwa kwao na kifo cha msanii huyo nguli wa bongo fleva ambaye amekuwa akiimba kwa kwa kutumia lafudhi ya kabila lake la Wamasai.
Aidha wameeleza kuwa kifo cha Mr.Ebbo ni pigo kubwa sana katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini na hata nje ya nchi kwani kazi zake nzuri zimewezesha utamaduni wa Taifa la Tazania kutangazwa kimataifa kutokana na staili aliyokuwa akiitumia ya kabila lake ambalo ni wenyeji wa Tanzania.
Kutokana na ujumbe uliokuwa ndani ya nyimbo zake hasa katika kuhamasisha maendeleo na kudumisha amani na umoja msanii huyu nguli amejizolea umaarufu mkubwa sana nchini jambo lililomfanya apendwe na watazania wote bila kujali kabila dini wala rangi.
“Sisi wakazi wa Iringa tumepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo cha msanii huyu maarufu kipenzi cha watanzania na kwa kweli kifo chake ni pigo kubwa sana kwa taifa letu kwani alikuwa ni mhamasishaji mzuri sana wa maendeleo katika taifa letu na aliuwakilisha vizuri sana utamaduni wa mtanzania kimataifa na kiukweli ataendelea kukumbukwa daima kwa mchango wake katika kuutangaza utamaduni wa mtanzania”anamalizia kusema Rahim Mdemu mkazi wa Kihesa manispaa ya Iringa.
Kwa upande wake Abeid Maila mwanafunzi wa Tumaini Iringa ameeleza kuwa Mr.Ebbo ataendelea kukumbukwa daima kwa bururdani yake nzuri aliyokuwa akiitoa na hasa kwa mtindo wa uimbaji wake kwa lafudhi ya kabila lake ,na pia ni pigo kwa tasnia nzima ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
“Kwa mara ya kwanza nimemfahamu Mr.Ebbo hasa alivyotamba na nyimbo yake ya kwanza ya “Mi mmasai bana”ambayo kimsingi ndiyo iliyomtoa hata hivyo nyimbozake wengi wanachukulia tu kuwa zinachekesha tu lakini hata kuelimisha.Kimsingi pengo aliloacha halitaweza kuzibika kamwe kwani hakuna atakayeweza kuiga staili ya uimbaji wake”
Kwa upande wa wanamuziki mkoani Iringa Mwanahabari halisi ilibahatika kukutana na Kijana mwanamuziki na msanii wa nyimbo za Hip hop mkoani Iringa anayefahamika kwa jina la Honorius Haule almaarufu kama Honorius. “Nitamkumbuka daima Mr.Ebbo kwa mchango wake mkubwa katika kukuza,kutangaza na kudumisha utamaduni wa mtanzania”alimalizia Honorius.
Mr.Ebbo amefariki mwishoni mwa wiki iliyopita katika hospitali ya misheni ya USA river iliyoko mkoani Arusha alikokuwa amelazwa kwa muda kidogo.
Subscribe to:
Posts (Atom)