.
Na John Alex.
Hivi karibuni watanzania tumeadhimisha miaka hamsini ya uhuru ikiwa ni tangu taifa hili lilipokombolewa kutoka katika mikono ya waingereza mnamo tarehe 9 mwezi disemba mwaka 1961 baada ya bendera ya wakoloni kushushwa pale kileleni mwa mlima Kilimanjaro na kusimikwa kwa bendera ya Taifa huru la Tanzania chini ya mwasisi baba wa taifa hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere ambaye kwa kushirikiana na wanaharakati wenzie walihakikisha kuwa taifa la Tanzania linakuwa huru na linatawaliwa na watanzania wenyewe.
Katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya TUMETHUBUTU,TUMEWEZA ,NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE wananchi wamekuwa wakitafakari kwa kina sana juu ya kauli mbiu hii kuwa ni nini tulichothubutu, ni nini tulichoweza na ni nini tunaendelea kusonga nacho mbele.Wengi wana mawazo na mitazamo tofauti .Hii inawezekana ni kutokana na itikadi zao za kisiasa ama kutofautiana tu kimtazamo kutokana na kile mtu anachoona na anachokiwaza kama sio anachokisikia.
Wasomi na wataalamu wa maswala mbalimbali walioboboea katika kufanya tafiti mbalimbali nchini wamejaribu kutoa ripoti za utafiti waliofanya na kutoa tathmini ya kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka hamsini tangu taifa hili lipate uhuru.Tathmini hizo zimegusa katika maeneo mbalimbali kama vile sekta ya afya, sekta ya elimu na maeneo mengi ambayo wataalamu hawa wamekuwa wakifanyia tathmini
.
Hata hivyo kwa mujibu wa tathmini na ripoti mbalimbali za wataalamu hawa wa maswala mbalimbali hapa nchini zimebainisha kuwa kiwango cha maendeleo kilichofikiwa hakilingani na umri wa miaka hamsini ya Taifa hili tangu lilivyokuwa huru.Kwa mfano tunapoangalia sekta ya elimu hususani swala zima la ufaulu wa wanafunzi yaani kiwango cha elimu kwa ujumla kimeshuka ukilinganisha na kipindi kilichopita.Tuachane nahayo kwani yanazidi kutukatisha tamaa
Ni dhahiri kuwa katika kipindi cha miaka yote hiyo ya uhuru hadi hivi leo,kuna mambo mengi ambayo watanzania kiukweli tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele.Kwa hayo hatuna budi kujipongeza na pia kuipongeza serikali iliyopo maarakani kwa kujitahidi kuthubutu,kuweza na mpaka sasa tunazidi kusonga mbele.
Wahenga wana msemo unaosema,Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Msemo huu una maana gani katika makala haya?Una maana kuwa,pamoja na mapungufu mengi tuliyoyaona na tuliyoyasikia kupitia vyombo vya habari kuhusu serikali, yapo mambo mazuri ambayo serikali kimsingi imeyafanya na ni sharti tuipongeze kwa uthubutu na kuonyesha kuweza.Lakini pia tunapaswa kujipongeza sisi wenyewe kwani sisi ndio walipa kodi kwa hiyo mafanikio hayo ni ya kwetu sisi hayainufaishi serikali peke yake
.
Leo nitumie fursa hii kuwaomba watanzania wote bila kujali itikadi zao za kisiasa kuwa wakweli na wawazi hasa tunapoangazia katika swala zima la miundombinu ya barabara.Kwa wale wazee wa mwaka sitini na moja ni nani wakati ule alijua kuwa angeweza kusafiri kutoka Tanga hadi Iringa kwa masasa nane tu?Ni nani wa wakati ule aliamini kuwa ipo siku Tanzania itaunganishwa na barabara za lami kwa kila mkoa?Ni nani aliamini kuwa ipo siku barabara za lami zitafika hadi vijijni?Utakapofanya utafiti utagundua kuwa wengi wahakuamini kuwa ipo siku Tanzania hii itakuwa na barabara kuu nzuri zenye kupendeza na zenye kiwango kinachotakiwa.
Leo hii kutoka Dar es salaam hadi Mbeya unahesabu masaa tofauti na kipindi kile ambapo barabara hizi zilikuwa za vumbi na zenye kutisha na yeyote anayesafiri kati ya mikoa hiyo miwili afikapo mlima Kitonga basi roho mkononi na sala zote huzisalia hapo akihofia kuwa huenda ndio mahala atakapofia kutokana na ubaya wa barabara iliyokuwepo kipindi kilichopita.
Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete imethubutu ,imeweza na inazidi kusonga mbele katika swala la miundumbinu ya barabara kwani hakuna awamu nyingine yeyote iliyopita ambayo imepata mafanikio makubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara zaidi ya awamu ya Rais Kikweteukweli ni huo.
Mikakati haiishii hapo tu bado ujenzi wa barabara za lami unaendelea kwa kasi ndani ya mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwa ni barabara za kuunganisha wilaya ndani ya mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.Haya ni mafanikio makubwa sana yaliyopatikana katika kipindi hasa cha awamu ya nne ya Rais Kikwete.Hapa turejee kauli mbiu yetu ya maadhimisho,TUNAZIDI KUSONGA MBELE.
Leo wananchi kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha miundombinu ya barabara tuthubutu kusema kuwa tutamkumbuka daima Rais Kikwete kwa kuimarisha miundombinu na si vinginevyo kwani hata kama kuna atakayefuata baada ya yeye bado yeye ndio atakuwa amefungua njia kuelekea mafanikio zaidi katika swala zima la miundombinu ya barabara.
Tukirejea hotuba ya Mh.Rais Kikwete wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru katika viwanja vya uhuru pale jijini Dar es salaam kwa ufupi tu, alisisitiza sana kuwa mafanikio yaliyopatikana katika swala zima la miundombinu ya barabara nchini ni jambo kubwa sana la kujivunia kama taifa changa linaloendelea.
Rais Kikwete alibainisha kuwa hali ilvyokuwa baada ya wakoloni kuondoka kwa upande wa miundombinu ilikuwa si ya kuridhisha hata kidogo kwani barabara za lami zilikuwa chache kama hakuna kabisa.
Hii ina maana gani? Barabara chache zilizokuwepo zilikuwa ni kwa ajili ya kusafirisha malighafi kutoka kwenye maeneo ya mashamba hadi bandarini ili kusafirisha malighafi nje ya nchi kwa hiyo hazikulenga kamwe kuwanufaisha wananchi wa Tanzania bali wao wenyewe mabepari ambao walikuwa wakitunyonya
Lakini leo barabara za lami mpaka vijijini zinajengwa mfano hai ni mkoani Kilimanjaro ambapo baadhi ya barabara za vijini zimejengwa kwa kiwango cha lami sio tu Kilimanjaro bali na maeneo mengi sana ya Tanzania, barabara za baadhi ya vijiji ni za kiwango cha lami.
Madaraja makubwa ya kuunganisha barabara hizi za kisasa yamejengwa na yaliyokuwa ya zamani yameimarishwa na kuwa ya kisasa.Mfano hai ni daraja la Mkapa lililojengwa katika kipindi cha mwishoni mwa wamu ya tatu ya Rais Mkapa, ambaloni daraja kubwa la mto rufiji.Achilia hilo kuna daraja la mto Ruvu ambalo limebadilishwa na kuimarishwa.
Ni wakati muafaka sasa baada ya kuadhimisha miaka hamsini na kutafakari kwa kina juu ya mafanikio namapungufu yaliyopatikana katika miaka hamsini ya uhuru kuachana na kutafakari mapungufu ,na kujikita zaidi katika kujua ni kwa namna gani sisi kama watanzania tunafanya nini ili kutokomeza yale mabaya nakuendeleza zaidi mazuri yaliyofikiwa japo si kitu kwa baadhi ya watu wachache wenye maslahi binafsi na chuki dhidi ya taifa letu na serikaliiliyoko madarakani ka ujumla.
Aidha ni jukumu la serikali kusahihisha mapungufu yaliyokuwepo na kuhakikisha kuwa inajipanga katika kuimarisha na kuboresha zaidi yale mafanikio mazuri ya kuridhisha yliyofikiwa katika kipindi chote walichopo madarakani na pia kuendeleza juhudi za kuimarisha mambo yote yanayoihusu kama serikali.
Pia ni jukumu la serikali kuhamasisha wananchi hususani maeneo ya kijijni kushiriki kiamilifu katika shughuli za kimaendeleo ambazo kimsingi ndizo zitalifanya taifa letu liendelee na kufikia katika kilele cha mafanikio.
Tuungane kwa pamoja katika kupiga vita maadui wanaoliyumbisha taifa hilli ambao ni ujinga maradhi na umasikini uliokithiri miongoni mwa watanzania ambao kimsingi ndio vita kuu katika taifa letu.Miaka hamsini ya uhuru tuungane kwa pamija watanzania huku tukirejea kauli ya tumesubutu,tumeweza,na tunazidi kusonga mbele katika vita dhidi ya umasikini.MIAKA HAMSINI YA UHURU,TUMETHUBUTU TUMEWEZA,NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE.
No comments:
Post a Comment