Sunday, December 4, 2011

Wakaazi wa Iringa wamlilia Mr.Ebbo.


Na John Alex.
Wakazi wa mkoa wa Iringa  na vitongoji vyake,wameeleza hisia zao kwa masikitiko kufuatiwa kifo cha msanii wa nyimbo za bongo fleva,mtayarishaji  na mmiliki wa studio ya Motika record  iliyoko mkoaniTanga Abel Motika  almaarufu kama Mr.Ebbo.

Wakizungumza na  Mwanahabari Halisi kwa  nyakati na amzingira tofauti  wananchi hao hususan  vijana wameelezea kushtushwa kwao na kifo cha msanii huyo nguli wa bongo fleva ambaye amekuwa akiimba kwa  kwa kutumia lafudhi ya kabila lake la Wamasai.

Aidha wameeleza  kuwa  kifo cha Mr.Ebbo ni pigo kubwa sana katika  tasnia ya muziki  wa kizazi kipya nchini  na hata nje ya nchi kwani  kazi zake nzuri zimewezesha   utamaduni wa Taifa  la Tazania kutangazwa kimataifa kutokana  na staili aliyokuwa akiitumia ya kabila lake ambalo ni wenyeji wa Tanzania.
Kutokana na ujumbe uliokuwa ndani ya nyimbo zake hasa katika kuhamasisha maendeleo na  kudumisha amani na umoja msanii huyu nguli amejizolea  umaarufu mkubwa sana nchini jambo lililomfanya apendwe  na watazania  wote bila kujali kabila dini wala rangi.

“Sisi wakazi wa Iringa tumepokea kwa masikitiko makubwa  sana taarifa za kifo cha msanii huyu  maarufu kipenzi cha watanzania na kwa kweli kifo chake ni pigo kubwa sana kwa  taifa letu kwani alikuwa ni mhamasishaji mzuri sana wa maendeleo katika taifa letu  na aliuwakilisha vizuri sana  utamaduni wa mtanzania  kimataifa  na kiukweli ataendelea kukumbukwa daima  kwa mchango wake  katika kuutangaza utamaduni wa mtanzania”anamalizia kusema  Rahim Mdemu mkazi wa Kihesa  manispaa ya Iringa.

Kwa upande wake  Abeid Maila mwanafunzi wa Tumaini Iringa ameeleza kuwa Mr.Ebbo ataendelea kukumbukwa daima kwa bururdani yake nzuri aliyokuwa akiitoa na hasa kwa mtindo wa uimbaji wake kwa lafudhi ya kabila lake ,na pia ni pigo kwa tasnia nzima ya  muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
“Kwa mara ya kwanza nimemfahamu Mr.Ebbo hasa alivyotamba na nyimbo yake ya kwanza ya “Mi mmasai bana”ambayo kimsingi ndiyo iliyomtoa hata hivyo nyimbozake wengi wanachukulia tu kuwa zinachekesha tu lakini hata kuelimisha.Kimsingi pengo aliloacha halitaweza kuzibika kamwe kwani hakuna atakayeweza kuiga staili ya uimbaji wake”

Kwa upande wa wanamuziki mkoani Iringa Mwanahabari halisi ilibahatika kukutana na Kijana mwanamuziki na msanii wa nyimbo za Hip hop mkoani Iringa anayefahamika kwa jina la Honorius Haule almaarufu kama Honorius. “Nitamkumbuka daima Mr.Ebbo kwa mchango wake mkubwa katika kukuza,kutangaza na kudumisha utamaduni wa mtanzania”alimalizia Honorius.


Mr.Ebbo amefariki mwishoni mwa wiki iliyopita katika hospitali ya misheni ya USA river iliyoko mkoani  Arusha alikokuwa amelazwa kwa muda kidogo.

No comments:

Post a Comment