Saturday, December 3, 2011

MR.EBBO,PENGO LISILOZIBIKA KATIKA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI.

                                                    ABEL MOTIKA,MR.EBBO






Jina kamili ni Abel Loshilaa Motika a.k.a Mr Ebbo, azaliwa tarehe 26 may 1974 jijini Arusha. Elimu ya msingi aliianza mwaka 1982 katika shule ya msingi kijenge baadae mwaka 1984 alihamia Tanga na kuendelea na masomo katika shule ya msingi nguvumali na kumaliza elimu ya msingi mwaka 1988.

Alijiunga na elimu ya sekondari katika shule iitwayo jumuiya sec school. iliyopo jijini Tanga. Alimaliza elimu ya sekondari mwaka 1992. Na kwa kipindi hicho chote wakati yuko shuleni alikuwa akiimba kwaya kanisani kwenye kanisa la kisosora (lutheran church) ambapo ilimsaidia sana kujifunza muziki.

Alirudi Arusha mwaka 1993 na kubahatika kupata kazi kwenye night club ambapo alitumia mishahara yake kurekodi nyimbo ambazo hazikumpa mafanikio yeyote isipokuwa zilimuweka katika ramani ya muziki.

Baada ya hapo alifanya kazi ya kuandaa matangazo ya biashara na vipindi vya redio kwenye studio iliyojulikana kama Supreme recording studios iliyopo mjini Arusha. kipindi hicho kilijulikana kama “Mambo gani haya”

Alirekodi nyimbo kadhaa ambazo hazikumpa mafanikio yoyote kwa mara nyingine na hali hiyo ikamkatisha tamaa kabisa.

Baadae mwaka 1995 alipata kazi ya kuuza nguo kwenye duka la JJ BLACK lililopo jijini Arusha. Mwaka 1999 aliamua kurudi jijini Tanga na akafanikiwa kufunga ndoa na kubahatika kupata watoto wawili Ashley na baadaye Alicia.

Alianza kazi ya uwakala wa kuuza magazeti mwaka 2000, kazi ambayo pia haikumletea mafanikio yeyote makubwa kama alivyokuwa anatarajia. Baadaye mwaka 2001 akaanzisha biashara ya kuuza mchele kwa jumla ambayo pia haikuwa na mafanikio aliyoyatarajia.

Kipindi hicho chote alipokuwa Tanga, alifahamiana na wasanii wa muziki wa Bongo Fleva,Professor J na Wagosi wa kaya, na wao pia walijua kuwa Mr. Ebbo ni msanii asilia.

Baadae alijiunga na chuo cha kozi za computer jijini tanga.Wagosi waliporekodi wimbo wao wa Tanga kunani ,Mr Ebbo alihamasika kurudi tena kwenye Muziki na ndipo alipoandika wimbo wa kwanza wa "Mimi Mmasai mwaka 2002". Wimbo huo ukatambulisha album yake ya kwanza kisha wimbo wa 'Fahari yako'. Baadaye mwaka 2003 akafungua studio ( MOTIKA RECORDS) ambayo ilifanikiwa kuwatambulisha wasanii kama Danny Msimamo, Dr Leader, Mo-Kweli, na wengineo wengi , wote hawa aliwaproduce yeye mwenyewe kama producer wa MOTIKA RECORDS.

Mwaka 2003 akarekodi Album yake ya pili iliyojulikana kwa jina la Bado Ijasungumiswa. Mwaka 2004 akarekodi Album yake ya tatu iliyoitwa Kazi gani. Mwaka 2005 akarekodi Album ya nne iliyoitwa Alibamu. Mwaka 2006 akarekodi Album ya tano inayoitwa Kamongo.ambayo ndio albamu ya mwisho kwa uhai wake.


BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA ,JINA LA MUNGU MUUMBA WETU LIHIMIDIWE DAIMA MILELE .AMEN!

No comments:

Post a Comment