Na John Alex.
Baaadhi ya wafanya biashara wa vyakula wenye migahawa na wafanya biashara zingine wanaofanya shughuli zao za biashara maeneo ya chuo kikuu Tumaini wamesema kuwa katika msimu huu wa sikukuu biashara ya vyakula na bidhaaa nyingine maeneo hayo ya chuoni imekuwa ngumu kupita kiasi.
Wakizungumza na Kwanza jamii kwa nyakati tofauti wafanya biashara hao wamesema kuwa, kufuatia likizo fupi chuoni hapo wanafunzi ambao ndio wanunuzi wakuu wa vyakula mahotelini na bidhaa nyingine wamekwenda majumbani kwao kusherehekea sikukuu ya krismasi hali inayopelekea kudorora kwa biashara na wengine kuthubutu hata kuzifunga kabisa kwa muda.
“Asilimia kubwa ya wateja wetu ni wanafunzi ambao wamekuwa wakinunua vyakula mahotelini kwa hiyo wanapoondoka inatulazimu wakati mwengine kufunga kabisa hoteli zetu kwani wanaobaki ni wachache ambao kati yao wapo wanaojipikia wenyewe” anasema Matata Elias .mmoja wa wafanya biashara mwenye mgahawa maarufu maeneo ya Tumaini ujulikanao kwa jina la Agape.
Aidha wafanyabiashra hao wamesema kuwa biashara ya vyakula na bidhaa nyingine maeneo hayo ya Tumaini huwa ni ya msimu ambapo wanafunzi wanapokuwa masomoni biashara huwa inachanganya na pindi tu wafungapo chuo wao hulazimika kufunga na hivyo shughuli za biashara kusimma kwa muda mpaka chuo kitakapofunguliwa.
Wafanya biashara hao wameongeza kuwa ugumu wa biashara chuoni hapo hususan kipindi hiki cha karibuni umechangiwa pia na kupanda kwa gharama za maisha ambapo wengi wa wanafunzi inawalazimu kubana matumizi kwa kujipikia wenyewe.
“Hata hawa wachache waliobaki hawatuungishi vizuri kwa kweli nadhani ni kwa sababu ya uchache wao na wengi kuwa wamekwenda likizo kwa hiyo wengi wetu inatulazimu kufunga biashara zetu kutokana na faida ndogo”anasema Hasani Lumato mmoja wa wafanya biashra wanaojihusisha na ukaangaji wa chipsi.
Hata hivyo kwa upande wa biahsara nyingine kama vile biashara za vifaa vya maofisini huwa ni kawaida yao pindi ifikapo muda wa likizo huwalazimu kufunga kabisa biashara zao kwani wanafunzi na wafanya kazi ambao ndio wanunuuzi wakuu wa bidhaa zao wanakuwa wamekwenda likizo na ambao wanabaki shughuli za masomo na kiofisi husimama.
Wanafunzi wa chuo cha Tumaini wamefunga likizo ndogo kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya krismas na wanatarajia kurejea masomoni mara baada ya sikukuu kuisha mwezi januari 2012.
No comments:
Post a Comment